Kesi dhidi ya unyanyasaji wa CIA kuendelea US

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi la Marekani CIA John Brennan

Jaji nchini Marekani ameruhusu kuendela kwa kesi inayohusu mateso yanafayonywa na shirika la ujasusi la Marekani CIA dhidi ya kile kinachotajwa kuwa vita dhidi ya ugaidi

Chama cha kutetea maslahi ya umma kiliwashtaki wanasaikolojia wawili kwa niaba ya waliokuwa wafungwa watatu wa CIA na kuwalaumu kwa kutoa mafunzo kuhusu mbinu za kutesa

Wakijitetea wanasaikolojia hao walisema kuwa walibuni programu hiyo lakini hawakuhusika kuitekeleza.

Zaidi ya wafungwa 100 walifanyiwa mbinu hizo za mateso ikiwemo kunyimwa usingizi, kumwagiwa maji na kupigwa.