Rais wa miaka 36 awania uchaguzi Equatorial Guinea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Teodoro Obiang Nguema ameongoza miaka 36

Rais aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi barani Afrika Teodoro Obiang Nguema, anatarajiwa kushinda katika uchaguzi mkuu wa unaoendelea leo Equatorial Guinea.

Rais Teodoro Obiang Nguema ambaye ameiongoza Equatorial Guinea kwa miaka 36 anashiriki katika uchaguzi huu akitarajia kuongezewa kipindi kingine.

Taifa hilo dogo linautajiri mkubwa sana wa mafuta.

Hata hivyo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi katika umasikini mkubwa.

Uchaguzi huu ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka uliopita lakini ukaahirishwa bila sababu mwafaka isipokuwa amri ya rais.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Bwana Obiang mara zote anapata angalau asili mia 95% ya kura.

Rais Teodoro Obiang ameongoza Equatorial Guinea, nchi yenye utajiri wa mafuta, kwa mabavu, tangu alipompindua mjomba ake, mwaka wa 1979.

Kuna wagombea wengine sita wanampinga, lakini vyama vikuu vya upinzani, vinasusia uchaguzi huo.

Bwana Obiang mara zote anapata angalau asili mia 95% ya kura.

Hata hivyo maelfu ya wapiga kura walijitokeza katika mji mkuu wa Malabo.

Matokeo ya uchaguzi huu yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa juma lijalo6