Lucy Kibaki afariki

Image caption Lucy kibaki na mkewe wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2007

Mke wa kwanza wa rais Lucy Kibaki amefariki katika hospitali mmoja mjini London kwa ugonjwa usiojulikana.

Lucy alipata umaarufu kwa kumchapa kofi mpiga picha mmoja mwaka 2005 wakati alipovamia afisi za kituo kimoja cha habari mwaka 2005 akikasirishwa na vile habari moja ilivyoandikwa.

Katika kumbukumbu ya kumuhenzi bi Kibaki rais wa Kewnya Uhuru Kenyatta alimsifu kwa jukumu lake kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini Kenya.

Image caption Lucy Kibaki pamoja na aliyekuwa mke wa aliyekuwa rais wa Marekani George Bush ,Laura Bush.Picha kwa niaba ya Getty Images

Bwana Kenyatta alimrithi mumewe bwana Kibaki ambaye alitawala kutoka mwaka 2002 hadi 2013.

Bi Kibaki aliyezaliwa mwaka 1940,alijiondoa katika maisha ya hadharani wakati wa mwisho wa utawala wa mumewe.

Image caption Lucy Kibaki na mumewe Mwai KIbaki wakiwapungia mkono wafuasi wao mda mchache baada ya kibaki kuwasilisha stakhabadhi zake za uchaguzi katika tume ya uchaguzi mwaka 2007.Picha ni kwa niaba ya Getty images

Mara ya mwisho kuonekana hadharani ni mwezi Agosti mwaka 2010,wakati alipofurahishwa na kupatikana kwa katiba mpya.

Image caption Lucy Kibaki na mumewe aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki pamoja na mkewe marehemu Kijana Wamalwa wakati wa misa ya kifo cha Wamalwa.Picha kwa niaba ya Getty Images

Bwana Kenyatta alisema kuwa alikuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo amekuwa akipata matibabu nchini Kenya na Uingereza.Bi Kibaki ni mwalimu ambaye aliwacha kazi yake kabla ya ndoa yake na kibaki mwaka 1962 ili kuwalea wanawe.