Watu 10 wamekamatwa kwa kuua Albino Malawi

Image caption Watu 10 wamekamatwa kwa kuua Albino Malawi

Polisi nchini Malawi wamewakamata watu 10 kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke mmoja mwenye ulemavu wa ngozi (Albino)

Mauaji hayo yametokea wakati ambapo ujumbe wa Umoja wa Mataifa upo nchini humo kutathmini hali ya usalama wa watu wenye ulemavu wa Ngozi.

Katika siku za hivi punde mauaji ya watu wenye Albino yamesababisha serikali kutoa amri ya kupiga risasi na kuua mtu yeyote anayewashambulia.

Kisa cha hivi punde kilimhusisha mwanamke mwenye umri wa miaka 21.

Image caption Kisa cha hivi punde kilimhusisha mwanamke mwenye umri wa miaka 21.

Polisi wanasema kuwa kesi 30 zimeripotiwa katika siku za hivi punde.

Visa hivyo vinajumuisha utekaji nyara, mauaji ,umiliki wa mifupa ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Katika visa kadhaa magenge hayo haramu yanawatumia jamaa za watu wenye Albino kuwateka kuwajeruhi na hata kuwaua.

Kisa cha mauaji ya mtoto mwenye umri wa miaka 2 yaliibua hamaki kote nchini.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yamkini mifupa ya Albino hutumiwa kutekeleza matambiko yanayoambatana na itikadi za kitamaduni nchini humo.

Babake mzazi ni mmoja kati ya washukiwa wakuu.

Yamkini mifupa ya Albino hutumiwa kutekeleza matambiko yanayoambatana na itikadi za kitamaduni nchini humo.

Shirikisho linaloshughulikia maswala ya Albino APAM linawalaumu waganga wa mitishamba kwa kueneza dhana kuwa sehemu za mili ya Albino zinaweza kuwasaidia kusuluhisha matatizo yao ikiwemo kuwapa utajiri mkubwa.

Majuzi watu waliokuwa na hamaki waliwakamata washukiwa wakuu 7 wa mauaji ya Albino na kuwachoma moto kusini mwa Malawi.