IS ladai kutekeleza shambulio la kwanza Somalia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Islamic State

Kundi la wapiganaji wa Islamic State limekiri kutekeleza shambulio lake la kwanza nchini Somalia.

Linasema kuwa wapiganaji wake walilenga vikosi vya Umoja wa Afrika katika shambulio la bomu mjini Mogadishu.

Islamic State limejaribu kujiimarisha nchini Somalia lakini limeshindwa kutokana na uwepo wa kundi la Alshabab,likiwa mshirika wa kundi pinzani la Al-Qaeda.

Taarifa hiyo kutoka IS haikusema ni lini shambulio hilo lilitekelezwa ama iwapo kulikuwa na majereha yoyote.

Wakati huohuo serikali ya Somalia imesema kuwa imemkamata kamanda mmoja wa kundi la IS aliyetoroka katika kundi la Al-Shabab ambaye amekuwa akitafutwa.

Kundi la IS limekuwa likitafuta uungwaji mkono kutoka kwa makundi ya wapiganaji nchini Somali kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa lengo la kuchukua udhibiti wa eneo la Afrika mashariki.