Simba 30 kupelekwa Afrika Kusini

Simba Haki miliki ya picha AP
Image caption Simba hao watasafirishwa Ijumaa

Simba zaidi ya 30 ambao wameokolewa kutoka kwa makundi ya wanasarakasi Peru na Colombia watahamishwa na kupelekwa Afrika Kusini.

Wanyama hao waliokuwa wanatumiwa na wachezaji wazungukao mjini kuonyesha michezo yao waliteswa na kudhalilishwa, kwa mujibu wa kundi la kutetea haki za wanyama la Animal Defenders.

Haki miliki ya picha AP

Simba mmoja alipofuka.

Wengine wengi walikatwa kucha zao.

Haki miliki ya picha AP

Kundi hilo la Animal Defendersndilo lililopanga shughuli hiyo ya kuwasafirisha wanyama hao.

Ndiyo shughuli kubwa zaidi kuwahi kuandaliwa ya kuwasafirisha simba.

Haki miliki ya picha AP

Simba hao watafungiwa kwenye vizimba kama hivi na kusafirishwa Ijumaa.