Mauzo ya magari ya Mitsubishi yapungua

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mitsubishi

Kampuni ya kuunda magari ya Japan, Mitsubishi inasema kuwa ununuzi wa magari hayo katika soko la Japan umepungua kwa nusu baada kuibuka wiki iliyopita kuwa ilidanganya kuhusu majaribio ya matumizi ya mafuta.

Hata hivyo rais wa Mitsubishi Tetsuro Aikawa alisema kuwa aliona hakukuwa na sababu ya kuomba msaada wa kifedha.

Siku ya Jumanne kampuni hiyo ilikiri kuwa mfumo uliotumiwa kudanganya kuhusu matumizi ya mafuta umetumika kwa kipindi cha miaka 25 na kampuni hiyo haifahamu ni magari mangapi yaliyoathiriwa.