Kuishi na ndovu barani Afrika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Idadi ya ndovu inazidia kupungua Afrika
Katika kijiji kimoja kilichopo kando kando mwa mbuga ya kitaifa nchini Kenya, watu wanaomboleza kifo cha mtoto wa miaka 10 Tippape. Alikuwa akihudumia ng'ombe mbele ya nyumba yao Jumamosi moja wakati aliposhambuliwa na ndovu, alikanyagwa na kuuawa.

Kijiji kizima kilicho cha jamii ya Wamaasai kilibeba mikuki na kundi la watu 200 walielekea msituni kumtafuta ndovu huyo.

Ndovu wawili wakubwa waliuawa na wengine walijeruhiwa vibaya. Mtoto mmoja wa ndovu aliachwa yatima baada ya mamake kuuawa.

Jamii inafahamu faida inayotokana na ndovu hao, kutokana na kuwasili kwa watalii napia fedha wanazopokea kwa kukodisha ardhi yao.

Lakini wakati uhai unapohatarishwa au mimea kuharibiwa ni lazima umauzi mgumu uchukuliwe.

Kuna tofauti kubwa kati ya jinsi watu wa mataifa ya magharibi wanavyowachukulia Ndovu, kupitia mambo kama vile safari za mbugani au vipindi kuhusu wanyama pori, ikilinganishwa na fikra ya wanaoishi na wanyama hao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pembe za ndovu zikiteketezwa moto kusitisha biashara hiyo haramu

Na katika siku zijazo idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka.

Idadi ya Waafrika itaongezeka mara mbili kutoka bilioni moja hadi bilioni mbili katika miaka 20 ijayo na ni lazima wapate mahali pa kuishi, sehemu watakayoweza kupanda mimea ya chakula na sehemu ya mifugo yao kula nyasi.

Ulaya iliangamiza misitu yake mikubwa na uwepo wa wanyama pori karne kadhaa zilizopita, na kuna unafiki katika kuiomba Afrika ilinde misitu na wanyama pori wake kwa minajili ya kukuza uchumi.

"Iwapo tutakuwa ni wa kuiomba Africa itunze maeneo yake kwa wanyama," anasema Tom Milliken wa Traffic, "huedna dunia italazimika kugharamia hilo, au rasilmali zilizopo - wanyama walio hai - watalazimika kuligharamia hilo kwa namna fulani."

Kuna tatizo jingine pia, kwa binaadamu na ndovu pia- kuharibika kwa mazingira kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakati hali hiyo inaongezeka ushindani wa kutafuta nafasi unaongezeka pia.

Idadi ya ndovu inapungua kwa kasi

Miaka 100 iliyopita kulikuwa na kiasi cha ndovu milioni kumi Afrika. Hii leo kuna kiwango kisichozidi nusu milioni na idadi hiyo inapungua kwa kasi kubwa.

Hawato tokomea kabisa katika kizazi chetu, lakini uwepo wao utapungua kwa kiwango kikubwa.

Hali mbaya zaidi huenda kukawepo ndovu laki moja watakaokuwa katika maeneo yanayolindwa Africa yaliozungushwa ua huku kukiwepo maafisa wa kushika doria watakaokuwa wakihakikisha kwamba wawindaji haramu hawaingi," anasema mchambuzi wa masuala ya mazingira Esmond Bradley Martin.

"Ni jukumu la serikali kuamua ni kiwango kipi cha ardhi inataka kuwatengea ndovu."

Kiasi ya ndovu nusu waliosalia Afrika wanazunguka katika maeneo yalio na idadi ndogo ya watu huko Kavango Zambezi Transfrontier Conservation - eneno la mpaka lililo na ukubwa kama Ufaransa linalotumika kati ya Angola, Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe.

Shughuli mpya ya kuhesabu ndovu waliopo na idadi hiyo kutarajiwa kuchapishwa mwaka huu inatarajiwa kuonyesha idadi nzuri katika eneo hilo na katika baadhiya maeneo mengine kuna idadi kubwa zaidi ya ndovu.

Lakini katika maeneo mengi- yaani Garamba na Tanzania - idadi ya ndovu inapungua.

Zimbabwe, kwa mfano, inakabiliwa na matatizo wakati kemikali aina ya cyanide kutoka machimbo ya madini inawekwa kwa makusudi katika visima kuwaua ndovu ili wang'olewe pembe zao - inamaliza wanyama wengine pia.

Lakini katika baadhi ya nchi kumebuniwa njia kufanya ndovu kuwa na thamani zaidi wakiwa hai kuliko wakiwauawa.

Kikosi cha jeshi cha Garamba inadhaminiwa na wafadhili, kwasababu watalii hawafiki kupumzika katika maenoe yanayogubikwa na vita. Lakini mbuga zinazosimamia eneo la Garamba, zimepiga hatua kubwa katika mojawapo ya mbuga zake nyengine huko Chad.

Uwindaji ndio uliotoa thamani ya ndovu Namibiana uwajibikaji mkubwa unahakikisha kuwa fedha zinakwenda zinakostahili kufika.

Suluhu ya nchi moja sio suluhu kwa nchi nyingine, ambapo kuna tofauti ya viwango vya ufisadi na mitazamo tofuati dhidi ya wanyama pori na misitu.

Kupunguza haja ya pembe za ndovu na kukabiliana wasafirishaji haramu wa pembe hizo ni baadhi ya mambo makuu, ambapo bila ya hayo wawindaji wataelekea katika nchi ambapo inawezekana kuendesha shughuli zao na kupata pembe hizo bila ya kukamatwa.