Faly Ipupa na mashabiki waulaki mwili wa Papa Wemba

Image caption Faly Ipupa

Baadhi ya watu maarufu waliowasili kuulaki mwili wa mawanamuziki nyota katika uwanja wa ndege nchini DRC ni Pamoja na mwanamuziki mashuhuri Faly Ipupa pamoja na mtu anayemwigiza aliyekuwa rais wa DRC Mobutu Seseseko.

Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.

Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Image caption Mwili wa Papa Wemba

Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous.

Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.