Kim Jong un,Donald Trump,Nicki Minaj wana ushawishi mkubwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kim Jong Un

Nicki Minaj,Kim Jong un Donald Trump na Lewis Hamilton wana kitu kimoja kinachowaunganisha.

Huwezi kufikiria kwamba wanaweza kuketi katika meza moja ,lakini wametajwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani.

Orodha hiyo ya mwaka 2016 pia inamshirikisha Hillary Clinton,Kendrick Lamar, PewDiePie, Adele,Caitlyn Jenner na Leonardo DiCaprio.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump

Katika tamasha la siku ya Jumanne la New York baadhi ya nyota hao walihudhuria.

Nicki alisema kuwa hiyo inatokana na yeye kuwa mwanamke huru.

Aliwambia wanaume waliojaa katika ukumbi wa tamasha hiyo kwamba :iwapo hamjui kuwashughulikia wanawake wenu kuna watu 100 ambao wana uwezo wa kuchukua fursa hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nicki Minaj

Lewis Hamilton alisema kuwa ni heshima kubwa kwake kuorodheshwa katika tamasha hiyo ya watu 100 mbali na kuorodheshwa miongoni mwa watu 100 duniani walio na ushawishi mkubwa.

Wakati huohuo alimuomboleza marehemu Prince akisema kuwa alikuwa mwanamuziki bora wa kizazi chote.