Huwezi kusikiliza tena

Video: Wasifu wa Papa Wemba

Wapenzi wa muziki kote barani Afrika wanaendelea kuomboleza kifo cha mwanamuziki maarufu Papa Wemba.

Gwiji huyo wa muziki wa Soukus aliaga dunia mwishoni mwa juma alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake katika tamasha la muziki Abidjan ivory Coast.

Papa Wemba alifariki dunia akiwa na miaka sitini na sita.

Wanamuziki nyota duniani wamekuwa wakitoa salaam zao za rambirambi kwa mtu ambaye muziki wake uliwavutia na kuwahamasisha wanamuziki na wapenzi wengi wa muziki kote barani Afrika.

Zawadi Machibya anaangazia wasifu wa mwanamuziki huyu nguli, Papa Wemba...