Msimu wa Dele Alli wakamilika, kunani?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Alli Dele

Kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli hatocheza tena msimu huu baada ya kupigwa marufuku ya mechi tatu kwa ukosefu wa nidhamu.

Alikiri mashtaka baada ya kamera ya runinga kumuonyesha akimpiga ngumi mchezaji wa West Brom Claudio Yacob katika tumbo.

Alli mwenye umri wa miaka 20 alipinga adhabu hiyo ya mechi tatu ,lakini ombi hilo lilikataliwa kulingana na shirikisho la soka nchini Uingereza FA.

Alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter akijuta na kusema:''Msimu wangu umeisha.Nisingefanya nilichokifanya''.

Aliongeza nimepata funzo na nitarekebisha kuimarika zaidi.

Kisa hicho cha dakika ya 26 hakikuorodheshwa katika ripoti ya refa siku ya jumatatu ambapo mechi ilikamilika 1-1.

Hatahivyo, ilishikwa na kamera