Ted Cruz apata fursa ya kupunguza uongozi wa Trump

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump na Ted Cruz

Gavana wa Jimbo la Indiana nchini Marekani amemuunga mkono mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Ted Cruz siku nne kabla ya mchujo muhimu katika eneo hilo.

Akifanya kampeni siku ya ijumaa,bwana Cruz alimpongeza Gavana Mike Pence,akisema kuwa atamuunga mkono.

Mchujo wa Indiana siku ya Jumanne ndio fursa muhimu ya Seneta huyo wa Texas kupunguza uongozi mkubwa wa Donald Trump.

Bwana Trump amejishindia idadi kubwa ya wajumbe na hivyo basi kukaribia kutajwa mgombea wa urais kwa niaba ya chama hicho.

Lakini Iwapo hatashinda wajumbe 1,237 kutukwa na mkutano wa chama cha Republican mnamo mwezi Julai.

Hatua hiyo itamaanisha kwamba ,wanaharakati na maafisa wakuu wa chama cha Republican watakuwa huru kumchagua mgombea mbadala Bwana Cruz ama John Kasich.