Wanaharakati Washia wavamia bunge Iraq

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bunge la Iraq

Wanaharakati wa Kishia wamevamia bunge wakipinga utata unaozunguka mkwamo wa kuidhinisha baraza jipya la mawaziri.

Mamia ya wafuasi wa kiongozi wa Shia, Moqtada al-Sadr walivunja milango ya kuingia bungeni baada ya wabunge kwa mara nyengine kushindwa kukutana ili kupitisha baraza hilo.

Bwana Sadr anamtaka waziri mkuu Haider al-Abadi kushinikiza kubadilishwa kwa mawaziri na wataalam wasiopendelea upande wowote.

Vyama vikuu katika bunge hilo vimekataa kuidhinisha mabadiliko hayo kwa wiki kadhaa.

Waandamanji hao waliwazuia wabunge waliojaribu kutoroka,''wakiimba waoga wanatoroka''.