Al Shabab waua wanajeshi 30 wa Somalia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Al Shabab waua wanajeshi 30 wa Somalia

Wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, Al Shabab wanasema wamewauwa wanajeshi wa serikali zaidi ya 30.

Al Shabab, wanadai kutekeleza mauaji hayo walipoteka tena kijiji cha Runorgood, Kaskazini-Mashariki mwa mji mkuu wa Somali Mogadishu.

Wenyeji wa kijiji hicho wamethibitishia BBC, kwamba kijiji chao kinadhibitiwa tena na wanamgambo wa Al Shabab.

Image caption Wenyeji wa kijiji hicho wamethibitishia BBC, kwamba kijiji chao kinadhibitiwa tena na wanamgambo wa Al Shabab.

Wapiganaji hao walikuwa wametimuliwa kutoka kijiji hicho hapo jana.

Kwengineko nchini Somalia, watu kama watatu waliuwawa, kwenye shambulio la bomu, katika soko la mifugo huko Qoryoolay, inavoelekea shambulizi hilo lililengwa maafisa wa kukusanya kodi wa serikali.