Maandamano ya Samaki Vietnam

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano ya Samaki yafanyika Vietnam

Kumetokoa maandamano yasiyo ya kawaida nchini Vietnam baada ya idadi kubwa ya samaki kupatikana wakiwa wamekufa pwani ya nchi hiyo.

Mamia ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi wakitaka serikali ya nchi hiyo ichukue hatua kali dhidi ya kampuni moja inayodaiwa kumwaga maji taka yenye sumu baharini na kusababisha idadi kubwa ya samaki kufa.

Waandamanaji wengine wamelaumu uchafuzi huo wa maji unaosababishwa na kampuni ya chuma ya Taiwan, Formosa Plastics.

Maandamano hayo yanafuatia ripoti ya serikali iliyoiondolea lawama kampuni hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano hayo yanafuatia ripoti ya serikali iliyoiondolea lawama kampuni hiyo.

Maandamano ya mji wa Hanoi nayo pia yalikuwa ya hasira kwa kile kinachooneka kuwa kujikokota kwa serikali kuchukua hatua za dharura kulinda mazingira na afya ya walaji wa samaki.

Samaki hao waliokufa walianza kupatikana wameelea baharini kuanzia mwezi uliopita.

Uchunguzi bado unaendelea kubaini nini hasa kilichosababisha idadi hiyo kubwa ya samaki kufa.