Iraq: Waandamanaji washia watashtakiwa

Haki miliki ya picha bb
Image caption Waziri mkuu wa Iraq ataka waandamanaji washia waliovamia bunge washtakiwe

Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ameamuru vikosi vya usalama kuwafikisha mbele ya haki waandamanaji ambao waliingia bungeni na kufanya msako.

Bw al Abadi anawataka waandamanaji waliowavamia walinda usalama pamoja na wabunge wakati wa maandamano ya siku ya Jumamosi ambao ni wafuasi wa muhubiri mbishi Moqtada al Sadr kukamatwa.

Mamia ya waandamanaji hao bado wamepiga kambi nje ya bunge mjini Baghdad.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji hao ni wafuasi kwa kiongozi wa dini mwenye siasa kali Moqtada al Sadr

ujio wao katika eneo lenye ulinzi mkali la Baghdad kunatishia usalama wa serikali inayolaumiwa na washia kwa utepetevu katika vita dhidi ya ufisadi uliokithiri nchini humo.

Wengi wa waandamanaji ni wafuasi kwa kiongozi wa dini mwenye siasa kali Moqtada al Sadr

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu bw al-Abadi amesema kuwa hali ya usalama mjini Baghdad imedhibitiwa.

Wamekasirishwa na kushindwa kuidhinishwa kwa mpango wa bwana Abadi, wa kuvunja mfumo wa ugavi wa mamlaka ambao umelaumiwa kwa kuchangia kuwepo ufisadi.

Waziri mkuu bw al-Abadi amesema kuwa hali ya usalama mjini Baghdad imedhibitiwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bw Abadi amesema kuwa kuwa mvutano uliopo unahujumu uwezo wa Iraq wa kupigana na kundi la Islamic State.

Wanaharakati wa Shia walivamia bunge wakitaka kuwepo mabadaliko ya kisiasa.

Bw Abadi amesema kuwa kuwa mvutano uliopo unahujumu uwezo wa Iraq wa kupigana na kundi la Islamic State.