Kenya:14 walifariki jengo la Huruma

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kenya:14 walifariki jengo la Huruma

Maafisa wa utawala nchini Kenya wanasema, kuwa watu 14 walikufa, wakati jumba la ghorofa sita lilipoporomoka Ijumaa, baada ya mvua kubwa kunyesha mjini Nairobi.

Shughuli za uokozi bado zinaendelea kutafuta walio hai chini ya kifusi.

Takriban watu 67 bado hawajulikani waliko , ingawa haijulikana kama walikuwamo ndani ya jengo wakati huo au la .

Maafisa wa serikali wanaendesha uchunguzi wa kubaini maafisa waliotoa idhini ya kujengwa kwa jumba hilo kwenye ukingo wa mto kinyume na kanuni za ujenzi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shughuli za uokozi bado zinaendelea kutafuta walio hai chini ya kifusi.

Vilevile mwenye jengo hilo bado mafichoni licha ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa amri akamatwe na kufunguliwa mashtaka.

Kutokana na hofu ya kuwepo kwa watu chini ya kifusi cha jumba hilo lililokuwa na wapangaji 198 maafisa wanaoshughulikia uokozi wamekataa kutumia matinga tinga kwa hofu kuwa huenda wakawaua manusura waliosalia mle chini.

Gavana wa Nairobi, Evans Kidero anasema maafisa waliotoa kibali kuhusu ujenzi wa jengo hilo, watatolewa makazini.