Polisi wa China kupiga doria Italia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wa China

Maafisa wanne wa polisi nchini China watashirikiana na wenzao wa Itali kupiga doria mjini Rome na Milan katika jaribio la wiki mbili.

Maafisa hao wanaozungumza Kitaliano wanatumwa nchini Itali kwa lengo la kuwafanya watalii wa China kujisikia huru na salama wakati huu wa msimu wa juu wa utalii,amesema waziri wa maswala ya ndani nchini humo Angelino Alfano.

''Iwapo jaribio hilo litafanikiwa,tutafanya hivyo kwa miji mingine nchini Italy'',alisema.

Takriban watalii milioni 3 wa China hutembelea Itali kila mwaka.

Bwana Alfano alisema kuwa maafisa wa Itali hivi karibuni wataanza kuelekea Beijing na Shanghai kupiga doria wakishirikiana na maafisa wa China.