Polisi Kenya wagundua njama za ugaidi

Image caption Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wamegundua njama za kupangwa kwa mashambulizi nchini humo na kundi moja la Afrika Mashariki lenye uhusiano wa karibu na IS.

Mwanaume mmoja,mkewe pamoja na mwanamke mwingine wamekamatwa na zawadi imetolewa kwa wanaume wengine wawili wanaoelezeka kama wenye silaha na hatari zaidi.

Polisi wanasema kuwa kundi hilo linajumuisha wataalamu wa masuala ya afya waliokuwa wamejipanga kutumia kimeta kama mpango wa shambulizi hilo kubwa.

Kundi hilo pia linashutumiwa kuhusika kuwaunganisha raia wa Kenya na makundi mengine yenye msimamo mkali nchini Libya na Syria.Haikuwa rahisi kuweza kupata uthibitisho wa suala hili.