''Mvulana wa Messi'' atorokea Pakistan

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Messi

Mvulana mwenye umri wa miaka 5 ambaye picha yake ilisambaa katika mitandao ya kijamii akiwa amevalia shati ya Lionel Messi ametorokea nchini Pakistan.

Babaake Murtza Ahmadi amesema kuwa alipata vitisho vya kutekwa nyara ikiwemo kutoka kwa wahuni waliokuwa wakitaka pesa.

Baada ya mvulana huyo kuwa maarufu kutokana na shati yake yenye mistari ya bluu,nyota huyo wa Argentina alimpatia jezi mbili alizozitia saini pamoja na mpira.''Nampenda Messi''.

''Ni mfalme'',Murtaza ambaya ana matumaini ya kuonana naye aliiambia BBC.Babaake Murtaza anasema kuwa waliondoka nyumbani kwao huko Ghazni kwa sababu hali ilikuwa hatari kwake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mvulana wa Messi

''Siku chache zilizopita nilipata simu kutoka kwa muhalifu mmoja .Aldhani kwamba kwa sababu mwanangu alipokea Tisheti hizo kutoka kwa Messi pia alipata pesa na hivyo akataka agawiwe'',Arif Ahmadi aliambia BBC.

Sasa familia inahisi kwamba Quetta itatoa makaazi mazuri kwa maisha ya Murtaza na ndugu zake saba ambao wote wanalala chumba kimoja.