Nigeria kupambana na wahamiaji haramu

Image caption Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Nigeria imesema inahitaji Euro bilioni moja kukabiliana na uhamiaji haramu nchini humo.Nchi hiyo ni kitovu cha wahamiaji kutoka Afrika wanaotaka kuingia Ulaya,ikiwa na zaidi ya wahamiaji laki moja wanaopitia katika nchi hiyo kila mwaka.

Waziri wa mambo ya nje wa Niger Ibrahim Yacouba alitoa pendekezo hilo mbele ya viongozi wenzake kutoka Ufaransa na Ujerumani walioitembelea nchi hiyo iliyopo Magharibi mwa Afrika.

Mwaka uliopita bara la Ulaya lilitoa zaidi ya Euro bilioni moja kwa nchi za Afrika Magharibi kukabiliana na suala la uhamiaji haramu lakini hii ikiwa ni kwa ukanda mzima.Viongozi wa Afrika wanasema fedha nyingi zaidi zinahitajika.