Mpinzani wa Donald Trump, John Kasich ajiondoa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mpinzani wa Donald Trump, John Kasich ajiondoa

Mpinzani mkuu wa Donald Trump katika kinyang'anyiro cha tikiti ya urais wa chama cha Republican , John Kasich amejiondoa mashindanoni.

Gavana huyo wa jimbo la Ohio ametangaza kusitisha kampeini zake baada ya kura ya maoni kuonesha kuwa umaarufu wake hauwezi kumpiku bwenyenye huyo mbishi anayepigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican kuwania urais wa Marekani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bw Trump anapigiwa upatu kutawazwa mgombea wa Republican.

Licha ya kushindwa kupata uungwaji mkono mkubwa wa wajumbe wa chama cha Republican, Gavana Kasich ameahidi kuwaomba rasmi wajumbe katika kongamano la kitaifa la chama hicho mwezi Julai.

Bw Trump anapigiwa upatu kutawazwa mgombea wa Republican.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bw Trump anapigiwa upatu kutawazwa mgombea wa Republican.

Kwa upande wake Kasich hakushinda jimbo lolote isipokuwa lake la Ohio.

Mpinzani mweza ambaye ni Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz naye alijiondoa mapema wiki hii kufuatia kushindwa kwake na bw trump katika jimbo la Indiana .

Gavana Kasich amefutilia mbali mikutano ya hadhara ya kampeini katika jimbo ya Washington. Mapema leo bw Kasich alizindua nembo yake iliyoundwa kwa mfano wa filamu maarufu ya Star-Wars ambapo alijieleza kuwa ndiye aliyesalia pekee yake dhidi ya Donald Trump.