Barack Obama ametembelea mji wa Flint

Haki miliki ya picha Reuters

Rais wa Marekani Barack Obama ametembelea mji wa Flint uliopo Michigan na kuwaahidi wakaazi wa eneo hilo kuwa maji safi na salama yatarejeshwa tena baada ya matatizo ya afya yaliyoikumba mji huo kutokana na uchafu wa risasi.

Obama amesema yeye pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali yake hawatalala mpaka pale tatizo hilo litakapotatuliwa.Obama alikunywa maji yaliyochujwa kuonyesha kuwa yalikua salama kwa matumizi.

Maji ya mji wa Flint yalichafuliwa na madini ya risasi baada wakati wa ubadilishaji wa vifaa vya maji mwaka 2014.