Urusi yakamata kundi la kigaidi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Urus Vladmir Putin

Mamlaka nchi Urusi imesema kuwa wamekamata kundi la watu kutoka Asia ya kati waliokuwa wanapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi mfululizo katika jiji la Moscow wakati wa kipindi cha likizo mwezi Mei.

Vyombo vya ulinzi nchini humo vimesema washukiwa walikuwa wanafanya matukio hayo kwa amri ya mashirika ya kimataifa ya ugaidi yaliyopo nchini Syria na Uturuki.

Imesema kiasi kikubwa cha mabomu pamoja na silaha zimekamatwa,lakini hawakutaja majina ama idadi ya watu walitiwa mbaroni.