Muziki wa Snura wapigwa marufuku Tanzania

Image caption Snura na albamu yake chura iliopigwa marufuku Tanzania

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku wimbo na kanda ya video ya muziki kwa jina chura wa msanii Snura Mushi kuchezwa katika vyombo mbalimbali vya habari hadi pale msanii huyo atakapoufanyia marekebisho wimbo huo.

Vilevile Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya mwanamuziki huyo hadi pale atakaposajili kazi zake katika baraza la taifa la sanaa BASATA.

Hatua hiyo inafuatia maudhui ya utengenezwaji wa video hiyo ambayo serikali inasema inakiuka maadili ya raia wa Tanzania.

Serikali imesema kuwa kazi ya mwanamuziki huyo inadhalilisha tasnia ya muziki nchini Tanzania.