Umoja wa Ulaya ilinde mipaka

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umoja wa ulaya wahimizana kuilinda mipaka yake.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewataka viongozi wa Ulaya kulinda mipaka ya nje ya umoja wa Ulaya ama kukiwa na hatari kila nchi itapaswa kujilinda yenyewe.

Katika mkutano na wanahabari pamoja na waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi mjini Rome,Merkel tatizo hilo ni changamoto kubwa kwa mustakabali wa mbeleni wa bara hilo.

Renzi amesema viongozi hao wawili wamepinga kwa pamoja mpango wa Austria kujenga ukuta katika mpaka wake na Italia.Austria inasema mpango huo ni muhimu kuzuia ongezeko la wahamiaji wanaoingia nchini humo wakitokea Italia.