Wakili mkosoaji akamatwa Misri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption rais wa Misri Abdul fatah el Sisi

Wakibili mmoja ambaye ni mwanaharakati wa kibinidamau amekamatwa nchini Misri ishara ya hatua ya serikali kukabiliana na wakosoaji wake.

Mwendesha mashtaka amemtaka kuzuiliwa kwa siku kumi na tano wakati madai dhidi yake yakichunguzwa.

Bwana Adly amekua mkosoaji mkubwa wa Rais Abdel Fattah Al-Sisi hususan baada ya Rais kutoa visiwa viwili katika bahari ya Shamu kama zawadi kwa Saud Arabia.

Pia ni moja wa mawakili ambao wamewasilisha kesi mahakamani kupinga hatua hiyo.

Adly alisifika sana wakati wa maandamano ya umma ambayo yalimuondoa madarakani Hosni Mubarak mwaka wa 2011.