Busu la Bieber na aliyekuwa mpenziwe lavutia Instagram

Image caption Justin Bieber akimpiga busu mpenziwe wa zamani

Picha ya mwanamuziki Justin Bieber akimpiga busu aliyekuwa mpenziwe Selena Gomez ndio picha iliopendwa na wengi katika mtandao wa instagram.

Imependwa na watu milioni 3,569,000 huku watu 350,000 wakiipenda dakika 15 tu baada ya kuchapishwa.

Image caption Justin Bieber akiwa kifua wazi

Picha hiyo iliokuwa na maelezo chini yake yalioandikwa ''Feels'' imeipiku picha ya Kendal Jenner ambayo ndio picha iliopendwa sana.

Pia nayo imezungumziwa karibu mara milioni.

Image caption Kendal Jenner

Picha ya nywele zake ilishinda mwaka 2015 na hivyo basi kuishinda picha ya dadaake Kim Kardashian ya harusi na Kanye West mwaka 2014.

Image caption Justin Bieber akiwa ndani ya ndege

Selena na Justin waliachana mwaka 2014 lakini mtandao haujamalizana na ''Jelena''.

Pia Bi Gomez aliipenda baada ya Justin Bieber kuichapisha.Justin Bieber sasa ana takriban wafuasi milioni 70 katika mtandao wa Instagram.

Image caption Justin Bieber akimshika chui milia

Picha yake ya hivi majuzi akimshika chui milia imependwa mara milioni mbili lakini haikuishinda picha ya Bieber aliyokifua wazi ambayo imependwa mara milioni 2.2.