Kenya kufunga kambi za Dadaab na Kakuma

Image caption Kambi ya Dadaab

Serikali ya Kenya inafunga idara zake zinazosimamia maswala ya wakimbizi katika hatua ambayo inatumai itaharakisha kufungwa kwa kambi kubwa za wakimbizi za Dadab na Kakuma.

Katika taarifa yake serikali inasema kuwa kuwahifadhi wakimbizi lazima kumalizwe.

Imeongezea kuwa wakimbizi 600,000 wengi wao wakitoka nchi jirani ya Somalia wanaishi nchini Kenya,na uhifadhi wao unaiathiri Kenya kiuchumi,usalama na kimazingira.

Serikali inahitaji usaidizi wa kimataifa ili kuwarudisha katika mataifa yao.