IS yakiri kuua polisi 8 mjini Cairo Misri

Haki miliki ya picha Manbar.me
Image caption IS yakiri kuua polisi 8 mjini Cairo Misri

Wanamgambo wa kundi la Islamic State wamedai kutekeleza shambulizi leo asubuhi lililosababisha vifo vya maafisa 8 wa polisi nchini Misri.

Kupitia mtandao wao wa mtandao wa kijamii wa Twitter Islamic State ilichapisha picha za miili ya maafisa wa polisi waliovalia mavazi ya kiraia.

Shambulizi hilo lililtokea katika kitongoji cha Helwan nje kidogo ya mji mkuu wa Cairo.

Wizara ya usalama wa ndani nchini humo awali ilitangaza mauaji ya maafisa hao 8 wa polisi.

Wizara hiyo ilisema kuwa watu wanne waliokuwa wamejihami kwa bunduki ndio waliotekeleza shambulizi hilo.

Haki miliki ya picha AFPGetty
Image caption Maafisa wa usalama wameanzisha oparesheni kuwasaka washambuliaji hao.

Maafisa wa usalama wameanzisha oparesheni kuwasaka washambuliaji hao.

Hakuna habari zaidi zilizotolewa na Serikali.

Kundi moja lililokuwa likitekeleza mashambulizi dhidi ya maafisa wa serikali ya Misri kwa muda mrefu liliapa uaminifu wake kwa kundi la wapiganaji wa Islamic satte mwaka wa 2014 na kuanzia hapo limepata nguvu zaidi na kutekeleza mashambulizi mengi na makubwa zaidi.

Hata hivyo wadadisi wa mambo ya usalama nchini Misri wanasema kundi hilo hsalikuwa na mazoea ya kushambulisha mji wa Cairo.