Maonyesho ya urembo wa ng'ombe India

Haki miliki ya picha AP
Mamia ya ng'ombe na fahali walitembea kwenye jukwaa mwishoni mwa juma katika mji uliopo kaskazini mwa India Rohtak katika maonyesho ya aina yake ya urembo.

Hafla hiyo iliandaliwa na serikali ya eneo hilo kutoa mafunzo kuhusu aina tofauati za ng'ombe na haki za mifugo hao.

Haki miliki ya picha AP

Zaidi ya ng'ombe 600 na fahali walishiriki na mmiliki ng'ombe aliyeshinda alijinyakuliwa zawadi ya dola 3,600.

Haki miliki ya picha AP

Wakulima waliwasili na mifugo yao kutoka wilaya za jimbo la Haryana na waliona fahari wakati ngo'mbe na fahali wao walipotembea juu ya jukwaa.

Haki miliki ya picha AP

Huku wengine wakitembea bila matataizo na kwa madaha wengine walibidi kusukumwa ili wamalize.

Haki miliki ya picha Manoj Dhaka

Mafahali walikaguliwa kwa uzito, sura na ukubwa wa pembe zao. Na ng'ombe walikaguliwa kutokana na uzuri wao na uwezo wao wa kutoa maziwa.

Haki miliki ya picha Manoj Dhaka

Waziri wa kilimo wa Haryana, OP Dhankar, alimtuza mmiliki ng'ombe aliyeshinda.

Wanafunzi wa taasisi ya kimataifa ya elimu na utafiti wa mifugo sehemu ambako maonyesho hayo yalifanyika, walipiga picha na ng'ombe walioshinda.