Mshukiwa wa ugaidi akamatwa Bamako

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ansar Dine ni kundi la wapiganaji wenye itikadi kali
Maafisa nchini Mali wanasema wamemkamata mwanamume anayeshukiwa kuhusika na mashambulio kadhaa ya kijihadi nchini humo katika katika nchi jirani Burkina Faso.

Yacouba Touré anashukiwa kuwa mfuasi wa kundi lenye itikadi kali Ansar Dine, linaloshirikiana na al-Qaeda.

Taarifa ya serikali inasema Yacouba Touré amehusishwana mashambulio kadhaa sio tu kusini mwa Mali bali pia Burkina Faso.

Anaaminika kuwa mojawao ya makamanda katika tawi la kusini la kundi hilo la Ansar Dine.

Ni mojawapo ya makundi yenye itikadi kali yanayodaiwa kushirikiana na kundi la kigaidi al-Qaeda lililodhibiti sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo kati ya mwaka 2012 na 2013.

Yacouba Touré pia anatuhumiwa kuwa mojawao ya wawasilishijai mkuu wa silaha kwa wafuasi wa itikadi kali kusini mwa Mali.

Maafisa wa usalama wanasema mwanamume huyo alikuwa akiishi katika mtaa karibu na uwanja wa ndege uliopo kwenye mji mkuu.