Raia Ufilipino wamchagua rais mpya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiga kura Ufilipino
Raia Ufilipino wanamchagua rais mpya na viongozi wengine.

Meya anayetambulika kwa uongozi wa kimabavu Rodrigo "Digong" Duterte ndio maarufu miongoni mwa wagombea watano licha ya matamshi yake wakatai wa kampeni yaliozusha mzozo kwa kuonekana kuwa na msimamo mkali.

Katika kampeni yake alitoa vitisho kuwaua maelfu ya wahalifu na kuahidi kuwaongoza kimabavu wabunge iwapo hawatomtii.

Wakosoaji wake wanaonya iwapo Duterte atashinda, atamaliza demokrasia ya miaka 30 Ufilipino.

Duterte ametuhumu kuwa serikali inapanga kuakikisha mgombea inayempendelea, Manuel Roxas anashinda.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mgombea urais Rodrigo "Digong" Duterte

Rais Benigno Aquino amekuwa akiongoza jitihada za kuwaunganisha wagmbea wengine ili kumshinda Duterte.

Ameonya iwapo Duterte atachaguliwa, basi nch hiyo itarudi katika utawala wa Udikteta.

Zaidi ya maafisa 100,000 wa polisi walitawanywa huku kukiwepo ghasia kabla ya uchaguzi.

Watu 10 wameuawa akiwemo mgombea wa U meya kusini mwa nchi hiyo.

Kampeni zimegubikwa na wasiwasi wa umma kuhusu uchumi, ukosefu wa usawa na ufisad unaokithiri katika nchi hiyo.

Kuna taarifa pia kwamba vituo vya kupiga kura huedna vikasalia wazi kwa saa zaidi katika baadhi ya maenoe baada ya kukabiliwana matatizo katika mfumo mpya wa uchaguzi wa elektroniki.

Jambo linaloarifiwa pia huedna likachelewesha kutangazwa kwa matokeo ya mwisho rasmi.