Michel Platini apunguziwa marufuku

Marufuku Haki miliki ya picha Getty
Image caption Platini sasa atatumikia marufuku ya miaka minne

Mahakama ya Kutatua Mizozo ya Kimichezo imepunguza marufuku aliyokuwa amepewa rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini na shirikisho linalosimamia soka duniani FIFA.

Mahakama hiyo imepunguza marufuku yake ya kutojihusisha na shughuli zozote za michezo kutoka miaka sita hadi miaka minne.

FIFA ilimpiga marufuku Platini pamoja na Sepp Blatter baada ya wawili hao kupatikana na hatia ya ukiukaji wa maadili.

Wote wawili wamekanusha kuhusika.

Platini anatarajiwa kujizulu wadhifa wake kama rais wa UEFA.