Kura ya kutokuwa na imani na Rousseff

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rousseff asema kura hiyo ni sawa na mapinduzi
Mpango wa kuamua kuidhinihsa kura ya kutokuwa na imani na rais wa Brazil Dilma Rousseff unaoenakana kuendelea kama ilivyopangiwa baada ya kaimu spika wa bunge la wawakilishi kubatilishi uamuzi wake kusitisha kura hiyo.

Spika Waldir Maranhao hakutoa sababu yoyote ya kubadili uamuzi huo.

Seneti sasa lintarajiwa kupiga kura Jumatano kuamua iwapo kuidhinisha kura hiyo ya kutokuwa na imani na rais Rousseff.

Awali spika Maranhao amesema kura katika bunge hilo ilioishia kwa wingi kuamua kuidhinisha kura hiyo ya kutokuwa na imani ilifanyika kimakosa na ni lazima irudiwe.

Haki miliki ya picha Agencia Camara
Image caption Spika Waldir Maranhao

Utetezi wa rais haukuzingatiwa kisawasawa na wabunge hawakupaswa kutangaza wazi msimamo wao kabla yakura, alisema Maranhao.

Wapinzani wa serikali wamesema Maranhao hana idhini kisheria kwa sababu suala hilo lishawasilishwa kwenye bunge la Seneti na wanahoji kuwa hawezi kupinga uamuzi uliopitishwa kabla ya yeye kuwa kiongozi wa bunge la wawakilishi.

Kila mtu Brasilia ameshangazwa na mtazamo huu mpya katika mzozo wa muda mrefu wa kisiasa akiwemo rais mwenyewe Dilma Rousseff.

Wiki iliyopita tu rais aliiambia BBC jinsi atakavyoendelea kung'anga'na kujitetea.

Iwapo kura hiyo itaidhinishwa kwenye Seneti ina maana rais Rousseff, atasimamishwa kazi kwa lazima kwa kipindi ambapo kesi dhidi yake itaendelea.