Kiongozi wa Kiislamu anyongwa Bangladesh

Haki miliki ya picha
Image caption Motiur Nizami

Kiongozi mmoja wa Kiislamu amenyongwa nchini Bangladesh kwa kutekeleza uhalifu wakati wa vita vya kupigania uhuru kutoka kwa Pakistan mwaka 1971.

Motiur Rahman Nizami mwenye umri wa miaka 73 alinyongwa mapema siku ya Jumatano kulingana na waziri wa sheria Anisul Haq.

Amepatikana na hatia ya mauaji ya kimbari,ubakaji na mateso.Nizami aliongoza chama kikuu cha Bangladesh ,Jamaat-e-Islam.

Mamia ya watu walikongamana karibu na jela yake katika mji mkuu wa Dhaka kusherehekea kunyongwa kwake.

Haki miliki ya picha BBC Bangla
Image caption Motiur Nizami akiwa mahakamani

Nizami ni kiongozi wa tano na mwenye mamlaka ya juu katika upinzani kunyongwa tangu mwezi Disemba mwaka 2013 kwa uhalifu wa kivita.

Bangladesh inasema upande wa mashtaka unahitajika kuponya vidonda vya mgogoro lakini makundi ya haki za kibinaadamu yanasema kuwa kesi hiyo haikuafikia viwango vya kimataifa.