Gordon Brown: Uingereza kusalia EU

Haki miliki ya picha
Image caption Alyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Uingereza Gordon Brown ameunga mkono kampeni za Uingereza kusalia katika muungano wa Ulaya akisema kuwa Uingereza haiwezi kujiweka kando kando ya Ulaya.

Brown alihoji kwamba Uingereza inahitaji kuwa katika muungano wa Ulaya ili kuongoza vita vya bara hilo dhidi ya ugaidi ,uhamiaji na mabadiliko ya tabia nchi.

Hatahivyo wanaopigania kujiondoa kwa Uingereza wanasema kuwa matamshi ya Gordon Brown haya msingi kwa kuwa alikuwa na rekodi mbaya alipokuwa mamlakani.

Raia wa Uingereza wataamua katika kura ya maoni ya June 23 iwapo watasalia katika muungano huo ama wataondoka.

Huku ikiwa imesalia wiki sita pekee hadi kufikia kura hiyo,kampeni ya kura hiyo imeimarishwa.