Modi mashakani kwa kufananisha jimbo na Somalia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Narendra Modi

Hatua ya waziri mkuu wa India Narendra Modi ya kulifananisha jimbo la Kerala Kusini na taifa la Somalia imewakasirisha wanasiasa na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Bw Modi siku ya Jumapili alisema katika mkutano wa kampeni za uchaguzi kwamba idadi ya watoto wanaofariki miongoni mwa kabila za jamii ya Kerala ni mbaya zaidi ya Somalia.

Watumiaji wa mtandao wa Twitter wamejibu kwa kuweka alama ya reli na neno PoMoneMod wakimshtumu Modi naye waziri Oommen Chandy akisema matamshi ya Bw Modi yalikuwa ''hayana msingi''.

Image caption Modi Kerala

Jimbo hilo linatarajiwa kupiga kura mnamo tarehe 16 mwezi Mei.

Chama cha Bharatiya Janata {BJP} kinachoongozwa na Bw Modi kimejaribu kutafuta kuungwa mkono katika jimbo hilo ambalo limekuwa likitawaliwa na chama cha Congress ama muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto.

Lakini matamshi yake ya hivi karibuni kutaka kuungwa mkono na wakaazi wa Kerala huenda yameambulia patupu.

Image caption Majibu ya watu katika mitandao ya kijamii

Somalia ina kiwango kikubwa cha watoto wanaofariki na wale wanaougua utapia mlo duniani,huku jimbo la Kerala likiwa na idadi ndogo ya watoto wanaofariki nchini India.

Bw Chandy alimuandika barua waziri mkuu akimtaka kuomba msamaha.