Justin Bieber: Sitapiga picha na mashabiki

Image caption Justin Bieber asema hatopiga picha tena na mashabiki wake

Iwapo hujagundua basi ujue kwamba nyota wa muziki wa Pop Justin Bieber yuko katika ziara ya ulimwengu.

Kwa sasa yuko nchini Marekani ambapo alionekana amepumzika katika mbuga moja kabla ya tamasha yake mjini Boston.

Image caption Bieber alivyoandika katika mtandao wa instagram

Bieber ambaye alikuwa hana viatu aliwavutia mashabiki lakini akakataa kuzungumza nao hadi watakapoweka simu zao chini.

Haijulikani iwapo picha alizochukua na mashabiki wake katika lango la mbuga hiyo zilikuwa za mwisho,lakini baadaye jioni alichapisha katika mtandao wake wa Instagram kwamba hatapiga picha tena na mashabiki.

Image caption Hivi ndivyo mashabiki wake walivyomjibu

''Iwapo utakutana nami mahali ujue kwamba sitapiga picha tena'',aliandika.

Alielezea vile watu hawaezi hata kumsalimia ama kujua kwamba hata yeye ni binaadamu na hivyobasi kumfanya kujihisi kama mnyama na sasa anataka kuheshimiwa.

Haki miliki ya picha twitter
Image caption Justin Bieber aiwa nchini Marekani

Aliongezea: Najua kwamba watu hawatafurahia lakini hakuna mtu anayenidai picha.