Wapendekezwa kuuawa misri

Haki miliki ya picha AP

Mahakama nchini Misri imependekeza adhabu ya kifo kwa watu 25 waliohusika katika mapigano ya kikabila kusini mwa nchi hiyo.

Kesi hiyo inayohusiana na mapigano kati ya ukoo wa kiarabu na kabila la Kinubi.

Zaidi ya watu 20 waliuawa katika ghasia zilizotokea miaka miwili iliyopita katika mkoa wa Aswan.

Polisi wanazielezea ghasia hizo kuwa ni mauaji mabaya ambayo hayaja wahi kutokea katika siku za hivi karibuni.