Kambi ya jeshi Nigeria 'sehemu ya kifo'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi limeapa kukabiliana na Boko Haram Nigeria
Shirika la kutetea haki za binaadamu Amnesty International linasema wafungwa wapatao 149 wamkufa katika hali mbaya katika kizuizi cha jeshi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka huu.

Katika ripoti, Amnesty linasema 11 kati ya waliokufa katika kizuizi cha Giwa walikuwa ni watoto wakiwemo watoto wachanga 4.

Limekitaja kizuizi hicho kama "sehemu ya kifo" na limesema kinapaswa kufungwa.

Jeshi halijatoa tamko lolote kuhusu ripoti hiyo ya hivi karibuni lakini katika siku za nyuma limesema limeidhinisha kitengo cha haki za binaadamu kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binaadamu.

Kizuizi kilichopo katika kambi ya jeshi ya Giwa kipo Maiduguri, mji mkubwa kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambako jeshilinakabiliana na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram.