Gari laingia katika shimo barabarani UK

Image caption Gari lililoingia katika shimo

Gari moja limeingia katika shimo kubwa katika barabara moja kusini mashariki mwa London.

Gari hilo aina ya Vauxhall Zafira liliwachwa katika mtaa wa Woodland Terrace mjini Charlton na Ghazi Hassan ambaye alikuwa akimtembelea nduguye siku ya Jumatano usiku.

Gari hilo la rangi ya buluu lilipatikana na maafisa wa polisi nje ya kanisa la St.Thomas mwendo wa 3.20 saa za Uingereza.

Image caption Gari lililoingia katika shimo

Mwandishi wa BBC mjini London amesema kuwa kuna uvumi kwamba huenda shimo hilo linatokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha mjini humo.

Nduguye Ghazi Abdul Ahmadzai alisema:Niliamka na mshtuko mkubwa .

''Maafisa wa polisi walikuwa hapa mapema asubuhi ,kwa hivyo nilitoka na kuona gari hilo ambalo walisema liko ndani ya shimo.Nilisema sina la kufanya na kurudi kulala,nimeamka tena''.

Image caption Gari lililoingia katika shimo

Alipoulizwa iwapo nduguye alikasirishwa na tukio hilo,Bw Ahmadzai alisema:''Hapana, anajua hakuna kitu anaweza kufanya,alitaka kujua iwapo kulikuwa na uharibifu.