Magomba
Huwezi kusikiliza tena

Magomba atumia mtandao kutetea albino Tanzania

Kufuatia Tanzania kuwa nchi iliyowahi kutokewa na mauaji ya mfululizo dhidi ya walemavu wa ngozi, albino na vitendo vingine vya ukatili, mlemavu wa ngozi Suleiman Magoma Magomba ameanzisha tovuti kama njia nyingine anayoamini itasaidia kutoa elimu na kukomesha vitendo hivyo vya mauaji.

Hata hivyo anasema hamasa ya kuanzisha wazo hilo aliipata baada ya kupata mwaliko maalumu kumtembelea Malkia Elizabeth wa Uingereza.

Na alizungumza na Mwandishi wa BBC Leonard Mubali.