Kamanda wa Hezbollah auawa

Haki miliki ya picha Reuters

Kundi la wapiganaji la Hezbollah limesema mmoja wa makamanda wake wa juu ameuawa.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Mustafa Badreddine ameuawa katika shambulio la anga la Israel nchini Syria.

Anasemekana kwamba alikuwa ni wa pili kwa cheo katika kundi hilo, baada ya kiongozi wake Hassan Nasrallah.

Alikuwa akidaiwa pia kuhusika na mauaji ya Waziri mkuu wa Israel Rafiq Hariri mwaka 2005.