Rihanna kuwalipia karo wanafunzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rihanna

Nyota wa muziki Rihanna amejitolea kufadhili elimu ya wanafunzi kupitia wakfu wake.

Hatua hiyo inaamanisha kwamba watu kutoka jamii zisizojiweza watapata msaada wa kulipa ada ya shule.

Wakfu huo wa Clara Lionel umekuwa ukifanya kazi tangu 2012 ambapo hutoa ruzuku kwa shule huko Barbados mbali na kuwasaidia wagonjwa wa saratani.

Image caption Nembo ya wakfu wa Rihanna

Bibiye Rihana alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani mwaka huo huo na hivyobasi kumfanya yeye kuanza kusaidia sekta ya matibabu.

Kwa sasa shirika hilo limepanuka na kutoa ufadhili wa elimu hadi kufikia dola 50,000 kwa wanafunzi waliopo Barbados,Brazil,Cuba,Haiti,Guyana,Jamaica na Marekani.

''Sidhani kwamba ni haki kwa watoto kubeba mzigo wa kifedha katika miaka walio nayo'',alisema Rihanna.