Temer ataka mabadiliko Brazil

Haki miliki ya picha AFP

Kaimu Rais wa Brazili Michel Temer amewataka raia wa nchi hiyo kuungana kuiondoa nchi hiyo katika matatizo makubwa yanayoikabili.

Katika hotuba yake ya kwanza, toka alipochukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Roussef, (ambaye amesimamishwa katika nafasi yake kwa tuhuma za kutumia madaraka vibaya), Temer amesema Brazil ni lazima ijenge tena sifa yake nje ya nchi hiyo kuweza kuvutia tena wawekezaji na uchumi wa nchi hiyo kukua tena.