Urusi lawamani kwa kudukua bunge la Ujerumani

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Ujerumani yailamu Urusi kwa kulidukua bunge lake na chama cha Angela Merkel

Shirika la ujasusi la Ujerumani BfV limeishtumu Urusi kwa kuhusika na misururu ya uhalifu wa mitandaoni katika mifumo ya kompyta za serikali ya Ujerumani.

Shirika hilo limesema kuwa kundi moja la uhalifu wa mitandaoni linalodaiwa kufanyia kazi serikali ya Urusi lilishambulia bunge la Ujerumani 2015.

Wiki hii imebainika kwamba wahalifu hao wanaohusishwa na kundi hilo hilo pia walilenga chama cha Christian Democrats cha Kansela Angela Merkel.

Urusi bado haijajibu hadharani shutma hizo zilizotolewa na shirika hilo la ujasusi BfV.