Kenya yaombwa kutafakari upya uamuzi wake

Haki miliki ya picha
Image caption Kambi ya wakimbizi ya Daadab
Serikali ya shirikisho Somalia imetaja hatua ya Kenya kutangaza kufunga kambi za wakimbizi kama yenye 'hatari' ambayo inaweza kuzidisha ugaidi kieneo.

Kauli hiyo inajri wiki moja baada ya serikali ya Kenya kusema imeanza mpango wa kufuinga kambi mbili za wakimbizi zinazowahifadhi zaidi ya wakimbizi laki sita- wengi wao kutoka Somalia.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje Somalia inaeleza hatua ya kufunga kambi hizo itakuwa na athari kubwa za kiusalama katika eneo zima la Afrika mashariki.

Kufungwa kambi hizo na kurudishwa kwa lazima wakimbizi hao kutatoa nafasi nzuri kwa makundi ya kigaidi kama Al shabaab kuwasajili watu, inasema taarifa hiyo.

Hili maafisa wa serikali wanasema, huenda likashinikiza shughuli za kigaidi katika eneo.

Haki miliki ya picha
Image caption Wakimbizi 10,000 walirudi kwa hiari Somalia kufuatia makubaliano ya pande tatu

Wanaiomba serikali ya Kenyakutafakari upya uamuzi wake kutoa nafasi ya kurudi kwa hiari wakimbizi hao - hatua inayotaja kuwa salama na ya ungwana zaidi.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa iwapo Kenya itaendelea na mpango wake huo, itakuwa a athari kwa hatua zilizopigwa katika vita dhidi ya ugaidi ambavyo vinategemea ushirkiano na kubadilishana taarifa za kijasusi.

Miaka 3 iliyopita, Kenya, Somalia na Umoja wa mataifa zilitia saini makubaliano ya pande tatu yaliosababisha zaidi ya wakimbizi 10,000 kurudi Somalia kwa hiari.

Mwaka huu, kambi hizo zimeadhimisha miaka 25 tangu kuundwa kufuatia vita vya kiraia Somalia.

Kenya inasema ina wasiwasi kuhusu usalama wake na inashutumu kambi hizo kutumiwa kama vituo vya kupanga shughuli za kigaidi.

Umoja wa mataifa na baadhi ya serikali za mataifa ya magharibi kwa pamoja zimetoa wito kwa Kenya kutofunga kambi hizo.