Mwanamuziki apigwa marufuku na Twitter

Image caption Azealia Banks

Mwanamuziki wa mtindo wa Rap Azealia Banks amepigwa marufuku na mtandao wa Twitter.

Nyota huyo wa 212 amezuiliwa kuingia katika mtandao huo kufuatia hatua yake ya kutumia mtandao huo kumtusi msanii Zayn Malik.

Ameshtumiwa kwa ubaguzi baada ya kufananisha mizizi ya mwanamuziki huyo mbali na kutumia matusi.

Image caption Zayn Malik

Kufuatia matamshi yake dhidi ya Zayn,ameondolewa katika tamasha la Born and Bred mjini London.

Gazeti la Metro limeripoti kwamba wizara ya maswala ya ndani nchini humo ilikuwa na mpango wa kumpiga marufuku mwanamuziki huyo kutoingia Uingereza.

Ukurasa wake wa Twitter kwa sasa unaonyesha kwamba amepigwa marufuku na kwamba akaunti yake imeondolewa katika mtandao huo.